Books in Swahili

Filter
Filter
Sort bySort Newest
  • by Line Kyed Knudsen
    9.95 kr.

    Lucy na Emma wanaenda kuendesha baisikeli na wanafunzi wengine wa darasa lake. Ghafla wanapotea msituni na Hassan. Anaendesha haraka ili kuwafikia wengine, lakini wanafikia njia panda ya barabara. Marafiki hao watatu hawajui ni barabara gani ambayo wanafunzi wengine wa darasa walikwenda. Watafanya nini?Mwandishi kutoka Uholanzi Line Kyed Knudsen (aliyezaliwa mwaka wa 1971) alijulikana mara ya kwanza na "Pigerne fra Nordsletten" mwaka wa 2003. Mnamo 2007 alipewa ruzuku ya Pippi kutoka kwa kampuni ya uchapishaji kule Uholanzi, Gyldendal. Yeye huandika vitabu vya watoto na vijana, na pia hufundisha mbinu za uandishi.

  • by Line Kyed Knudsen
    9.95 kr.

    Hatimaye Lucy anapata mtoto wa mbwa. Ni wa kuvutia, na yeye na rafiki yake Emma wanatarajia kucheza naye. Lakini anaruka na kuuma. Labda kupata mtoto wa mbwa haifurahishi sana kama Lucy alivyofikiria.Mwandishi kutoka Uholanzi Line Kyed Knudsen (aliyezaliwa mwaka wa 1971) alijulikana mara ya kwanza na "Pigerne fra Nordsletten" mwaka wa 2003. Mnamo 2007 alipewa ruzuku ya Pippi kutoka kwa kampuni ya uchapishaji kule Uholanzi, Gyldendal. Yeye huandika vitabu vya watoto na vijana, na pia hufundisha mbinu za uandishi.

  • by Line Kyed Knudsen
    9.95 kr.

    Emma atalala katika nyumba ya Lucy kwa mara ya kwanza. Amekuwa akitazamia siku hiyo yote. Lakini jioni hukumbuka mama yake. Labda anapaswa kwenda nyumbani?Mwandishi kutoka Uholanzi Line Kyed Knudsen (aliyezaliwa mwaka wa 1971) alijulikana mara ya kwanza na "Pigerne fra Nordsletten" mwaka wa 2003. Mnamo 2007 alipewa ruzuku ya Pippi kutoka kwa kampuni ya uchapishaji kule Uholanzi, Gyldendal. Yeye huandika vitabu vya watoto na vijana, na pia hufundisha mbinu za uandishi.

  • by Line Kyed Knudsen
    9.95 kr.

    Emma awakaribisha wanafunzi wenzake katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa. Ni sherehe ya kuvutia katika chumba cha kuchezea dansi chenye taa za disko na chakula kitamu. Sasa ni wakati wa Lucy kuwa na sherehe yake mwenyewe ya siku ya kuzaliwa. Lakini sherehe yake itakuwa ya kukata na shoka?Mwandishi kutoka Uholanzi Line Kyed Knudsen (aliyezaliwa mwaka wa 1971) alijulikana mara ya kwanza na "Pigerne fra Nordsletten" mwaka wa 2003. Mnamo 2007 alipewa ruzuku ya Pippi kutoka kwa kampuni ya uchapishaji kule Uholanzi, Gyldendal. Yeye huandika vitabu vya watoto na vijana, na pia hufundisha mbinu za uandishi.

  • by Jesper Nicolaj Christiansen
    20.99 kr.

    RONIN 1 - UPANGAMvulana anaamka katikati ya msitu. Hajitambui au kutambua jinsi alivyofika pale. Kwa usaidizi wa watu tofauti na wanyama, na pia mkuki ulio na uwezo wa kipekee, Ronin huyu anapitia matukio mengi. Wakati ambapo kijiji kinahitaji ulinzi wake, lazima ajifunze kupigana kwa heshima ya wakulima anaowaokoa, na kwa ajili yake mwenyewe.RONIN 2 - UTARonin anakutana na rafiki wa zamani na anaanza kujifunza kwa kutumia sensei wake, ambapo anajifunza kuwa hakuna lisilowezekana. Matukio yake yanakuwa mengi anapokuwa akiwatetea wanyonge na akiutumia uwezo wake vyema. Ronin anajifunza mengi kuhusu yeye mwenyewe, na inawezekana, pia kuhusu anakotoka.RONIN 3 - MKUKIRonin anakumbana na changamoto kali na kujifunza kuwa wakati mwingine, hata katika maadui, kuna mengi zaidi ya tunavyofikiri. Anapojifunza kuhusu maisha yake ya zamani, baba yake na mkuki, maswali mengi zaidi yanaibuka. Katika tukio la hivi karibuni, Ronin alikaribia kujua yeye ni nani na jinsi gani anaweza kuwasaidia wale wote anaowajali sana.RONIN 4 - KUCHARonin anaendelea na safari yake ya kuelekea Meifumado. Njiani, anashambuliwa na maadui ambao ni waovu zaidi kuliko chochote ambacho aliwahi kukutana nacho. Akiungana na marafiki zaidi, analazimika kufanya uamuzi mgumu na kuvishinda vikwazo vyake vigumu zaidi.RONIN 5 - KUONYESHAKatika sehemu ya mwisho ya mfululizo wa Ronin, Ronin anasafiri kwenda Meifumado kukutana na hatima yake na kuyaokoa maisha ya Azami. Ni kwa kupigana na Kivuli cha Mfalme na jeshi lake la mapepo wabaya ambapo Ronin anajifunza kuhusu mambo yake ya kale, familia yake na jinsi anavyoweza kutenda kulingana na jinsi alivyo na jinsi anavyoamini. Katika hali ngumu zaidi, lazima Ronin akumbuke jinsi shujaa wa kweli anavyopaswa kuwa.Mvulana anaamka msituni bila kukumbuka ya yeye ni nani au atokako. Kupitia mfululizo huu, Ronin anapitia matukio mengi ambayo yanamsukuma ukingoni. Njiani, anakutana na watu ambao wanamsaidia kukua na kujifunza mambo yaliyo muhimu. Kwa usaidizi wa mkuki wake wa ajabu na nguvu anazozipata kutoka kwenye mkuki huu, Ronin anapigana kwa wema. Kwa kila tukio jipya, Ronin anakaribia zaidi na zaidi kujitambua hakika yeye ni nani.Jesper Christiansen (b. 1972) ni mwandishi wa asili ya Kideni. Amehitimu katika Shule ya Uandishi wa Hadithi za Watoto na yeye huandika hadithi za matukio na za kubuni za watoto wa kila umri.

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    From 9.95 kr.

    Anne Larsen anatambua kuwa wakili yule wa utetezi aliyefariki alikatiza kazi yake muda mfupi tu baada ya kushindwa katika kesi, na kuwa mteja wake, ambaye alikuwa ni Patrick Asp aliyeua mtoto mdogo alikuwa amehukumiwa kufungwa jela. Baba yake wakili huyu wa utetezi ambaye alikuwa jaji wa mahakama ya juu ametoweka na hajapatikana alipo. Anne yupo kwenye jela ili kumhoji askari jela kuhusiana na mfungwa aliyefariki kutokana na kunywa dawa kupita kiasi, wakati Patrick Asp kwa usiri anaweza kumpa barua. Patrick Asp ameandika kuwa alifungwa kimakosa na kuwa mke wake alihusika katika kufanya hivi. Anne anamtafuta mwanamke huyu kwenye mkahawa anaoufanyia kazi. Pia anakutana na mwana wa mwanamke huyu, ndiye Bertram, na Anne anahisi kwamba wawili hawa wanaficha jambo. Kuna jambo lenye shauku kuhusu Uwe Finch pia, mwanamume ambaye mamake Bertam ana uhusiano naye. Anaonekana kama anayeficha kujitambua kwa hakika, na Anne anawasiliana na Roland Benito ili kutafuta msaada wake katika kutambua mwanamume huyu anaweza kuwa ni nani haswa.The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. Baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    From 20.99 kr.

    Bertram na marafiki zake watatu wameanzisha genge ndogo la majambazi linaloitwa The Hawks. Anaishi peke yake na mama yake, anayefanya kazi kama mhudumu hotelini. Hamkumbuki baba yake sana, kwa kuwa alikamatwa kwa makosa ya mauaji na kufungwa kifungo cha maisha Bertram akiwa umri wa miaka misaba pekee. Siku moja, Bertram aliiba jaketi ya ngozi ya bei ghali yenye chapa ya "Schott Made in USA" kutoka kwa mkahawa, ambayo ilimletea matokeo mabaya sana, na si kwa Bertram pekee. Rolando Benito, mpelelezi katika Mamlaka ya Malalamiko ya Polisi, na wenzi wake walitumwa ili kuwauliza maswali maafisa wawili wa polisi. Mlinzi wa gereza alikuwa ameruka nje ya dirisha lake katika ghorofa ya nne, huku maafisa hao wawili wakimvuta, baada ya malalamiko ya kelele nyingi iliokuwa ukitoka kwenye nyumba yake. Kwa kuwa mlinzi huyo wa gereza alikuwa baba ya rafiki wa shule wa mjukuu wa Rolando, yeye husikia uvumi kwamba mfungwa alikufa ndani ya gereza ambalo mtu huyo alikuwa akifanya kazi, na kwamba mlinzi wa gereza alihisi ametishwa na kuteswa. Kwa hivyo mwishowe hii si kesi ya kujitoa uhai? Anne Larsen, mwanahabari wa TV2 East Jutland, ako pia katika kesi hii. Kila mtu anaonekana kuwa na uhusiano na mfungwa mmoja, muuaji Patrick Asp, aliyeua mtoto wake mwenyewe mchanga na ni mfungwa katika gereza ambalo mlinzi huyu wa gereza alikuwa akifanya kazi. Vifo hivi vya kutatanisha vikiendelea kuongezeka, na hakimu wa Mahakama Makuu akipotea bila kugunduliwa, Rolando Benito na Anne Larsen wanaunganika wakitafuta uhusiano. Uhusiano huo unapatikana kuwa ni Bertram na wizi wa jaketi, na sasa Anne ako hatarini pia.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. Baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    From 9.95 kr.

    Anne Larsen anamuonyesha Roland picha ya Uwe Finch, na Roland kwa hakika haiwezi kuwa ni mwanamume yule anayemfanana, anatambua baadhi ya sehemu za uso wake. Kuna jambo kuhusu macho yake jinsi yamekaribiana sana. Ila haiwezi kuwa ni mwanamume yule anayefanana vile kwani alifariki miaka kadhaa iliyopita katika moto kwenye hoteli. Wakati mchoro wa vidole unatambua kuwa kwa hakika huyu ni mwanamume yule ambaye Roland alihofia kuwa ndiye, anapata azma ya kutambua ni kwa nini mwanamume huyu alirejea na kutambuliwa vingine na kwa nini anaweza kuwa katika eneo la Aarhus. Mama yake Bertram anapata jaketi iliyotengenezwa kwa ngozi iliyoibwa katika chumba cha Bertram na anataka kumrejeshea mpenzi wake. Kwa mara nyingine, Bertram anajaribu kumfikia na kumfanya aelewe kuwa maisha yake yako hatarini ila mama yake amekasirika na anakataa kumsikiliza. Mama yake anadai kuwa Bertram ana wivu tu na kuwa ni Bertram aliyemuua dada yake mdogo. Bertram amekasirika, anavuta sigara moja na kulala huku runinga ikiwa imewaka. Akiwa katika hali hii ya kulewa, kwa mara moja anagundua ukweli wa kutisha. Usiku unapoisha Bertram anagutuka kutoka kwa jhali ile ya kutunduwaza, anampata mama yake hajarejea nyumbani.The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. Baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    9.95 kr.

    Liv Løkke anafanya kazi kwenye duka la jumla la Netto lililoko Paderup, kama mhudumu katika eneo la kulipia. Anachukia mji huo, yeye mwenyewe, kazi yake, na maisha yake yasiyo na umuhimu; na hata hana haja ya kuwaangalia wanunuzi kujua ni akina nani. Anajua watu wengi kwenye eneo hilo na mitindo yao ya ununuzi. Lakini siku moja, inambidi amwangalie mteja fulani aliyenunua bidhaa ambayo ilimkumbusha maisha yaliyopita, na siku ile yenye mkasa ambapo alimuokoa kaka yake kutoka kwa nyumba iliyokuwa ikiteketea moto, baada ya mlipuko wa gesi kumuua mamake. Ni yeye... mpenzi wa mamake. Anadai kuwa na ushahidi kuwa kifo cha mama yake hakikuwa ajali.Inger Gammelgaard Madsen (alizaliwa 1960) ni mwandishi Mdenmaki. Awali Madsen alikuwa msanifu picha. Alianza uandishi kwa riwaya iitwayo, "Dukkebarnet" mnamo 2008 na tangu wakati huo ameandika vitabu kadhaa vya utanzu huo. Kati ya hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Zawadi ya Slangens" (2014), "Dommer og bøddel" (2015), "Blodregn" (2016) na "Msafishaji" (2019).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    9.95 kr.

    Anne Larsen, mwanahabari wa kituo cha televisheni cha TV2 East Jutland, anafuatilia kesi ya afisa kutoka Silkeborg ambaye inakisiwa aligongwa na mwenzake mbele ya nyumbani kwake. Hamu yake inaamshwa pakubwa na ajali ya moto ambayo alikuwa akichunguza kwa siri. Anaanza kuichunguza kwa karibu. Ni kwa nini Johan Boje alikuwa na shauku ya kesi hiyo? Ni kwa nini hangekubali tu ilikuwa ni ajali ya kuvuja kwa gesi?Inger Gammelgaard Madsen (alizaliwa 1960) ni mwandishi Mdenmaki. Awali Madsen alikuwa msanifu picha. Alianza uandishi kwa riwaya iitwayo, "Dukkebarnet" mnamo 2008 na tangu wakati huo ameandika vitabu kadhaa vya utanzu huo. Kati ya hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Zawadi ya Slangens" (2014), "Dommer og bøddel" (2015), "Blodregn" (2016) na "Msafishaji" (2019).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    9.95 kr.

    Baada ya kufanya kazi katika kipindi cha televisheni kuhusu maonyesho ya sanaa yatakayoanza mjini Rhanders, Anne Larsen anaamua kumtembelea Liv Løkke na kakake. Anapofika nyumbani mwake Liv, anauona mlango wa nyumba yao ukiwa wazi, na anahofia kuwa amefanyiwa jambo baya. Liv hayupo, lakini maovu ambayo Anne alikuwa anashuku yanathibitishwa. Ni sharti wampate muuaji huyo na kumzuia asifanye mauaji yoyote zaidi. Itakuwa ni changamoto yenye kuhangaisha kwa Anne Larsen, Roland Benito, na mfanyakazi mwenza.Inger Gammelgaard Madsen (alizaliwa 1960) ni mwandishi Mdenmaki. Awali Madsen alikuwa msanifu picha. Alianza uandishi kwa riwaya iitwayo, "Dukkebarnet" mnamo 2008 na tangu wakati huo ameandika vitabu kadhaa vya utanzu huo. Kati ya hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Zawadi ya Slangens" (2014), "Dommer og bøddel" (2015), "Blodregn" (2016) na "Msafishaji" (2019).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    20.99 kr.

    Johan Boje, msaidizi wa polisi wa Eneo la Kati na Magharibi mwa Jutland anafariki baada ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa kwa kasi akiwa nje ya nyumbani kwake usiku mmoja wa manane mwezi Machi. Bosi wake, Alex Borg, ni mmoja wa watu wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio. Kwa haraka anagundua kuwa hii si ajali ya kawaida ya kugongwa na gari na kisha mtuhumiwa kuhepa, lakini ni mauaji ya kikatili. Mwanake Boje mwenye umri wa miaka tisa anadai kuwa aliliona gari hilo, na kwamba lilikuwa linaendeshwa na afisa wa polisi. Je, ni fikra za kijana huyo mwenye mfadhaiko zinamchezea shere? Kamera ya uchunguzi ya kituo cha mafuta inathibitisha masimulizi ya mtoto – mtu fulani aliyekuwa amevalia sare za polisi alikuwa anaendesha gari hilo wakati wa usiku huo wa ajali ya mauti. Roland Benito, mpelelezi katika Mamlaka ya Malalamishi ya Polisi, anapewa usukani wa kuendesha kesi. Ni nani kati ya marafiki wa Johan Boje alikuwa na nia ya kutenda maovu kama hayo? Rolando Benito anaungana na Anne Larsen, mwanahabari kutoka kituo cha televisheni cha TV2 East Jutland. Wanafuatilia alama za magurudumu hadi kwenye moto, ambao ulikuwa na hasara kubwa kwa familia ya eneo hilo. Labda moto huo haukuwa ajali? Anne na Rolando wanakisia kuwa huenda nia ikawa ni tofauti sana na kile walichotarajia mwanzoni. Msako wa kumtafuta mhalifu huyo unaanza kabla hajafanya shambulizi lingine.Inger Gammelgaard Madsen (alizaliwa 1960) ni mwandishi Mdenmaki. Awali Madsen alikuwa msanifu picha. Alianza uandishi kwa riwaya iitwayo, "Dukkebarnet" mnamo 2008 na tangu wakati huo ameandika vitabu kadhaa vya utanzu huo. Kati ya hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Zawadi ya Slangens" (2014), "Dommer og bøddel" (2015), "Blodregn" (2016) na "Msafishaji" (2019).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    9.95 kr.

    Liv Løkke ana majinamizi, baada ya moto ule na maisha ya awali kuletwa kwa ulimwengu wake wa sasa. Anne Larsen anawasiliana naye. Mwanahabari huyo amemtembelea kakake, na ana hamu kubwa ya kutaka kujua kile alichotaka kutoka kwake, hata anakubali shingo upande kukutana naye kwenye hoteli moja mjini Rhanders. Lakini madai ya mwanahabari huyo yanamkasirisha sana; anaondoka hotelini humo akiwa na ghadhabu. Anapoona tangazo kwenye gazeti kuwa mwanawe Johan Boje alimuona muuaji, anaenda nyumbani mwake Johan Boje kukutana na mwanawe mbele ya mahali alipozikwa babake.Inger Gammelgaard Madsen (alizaliwa 1960) ni mwandishi Mdenmaki. Awali Madsen alikuwa msanifu picha. Alianza uandishi kwa riwaya iitwayo, "Dukkebarnet" mnamo 2008 na tangu wakati huo ameandika vitabu kadhaa vya utanzu huo. Kati ya hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Zawadi ya Slangens" (2014), "Dommer og bøddel" (2015), "Blodregn" (2016) na "Msafishaji" (2019).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    9.95 kr.

    Tume Huru ya Malalamishi ya Polisi haijui wapi pa kuanzia. Lakini baada ya kuwahoji bibiye Johan Boje na wenzake, Roland Benito amesadiki kuwa askari huo hakuwa bwana mwaminifu. Huenda muuaji alikuwa na nia zingine kando na zile wanazofuatilia. Wanamhoji mwanawe Johan Boje, Lukas, ambaye alikuwa karibu na mauaji zaidi ya ilivyodhaniwa awali. Upelelezi unachukua mkondo mpya pale ambapo Anne Larsen anapomtafuta Rolando. Anamwambia kile alichogundua, na kuwa anashuku kwamba shauku ya Johan Boje katika moto ule ilikuwa ni ya kibinafsi.Inger Gammelgaard Madsen (alizaliwa 1960) ni mwandishi Mdenmaki. Awali Madsen alikuwa msanifu picha. Alianza uandishi kwa riwaya iitwayo, "Dukkebarnet" mnamo 2008 na tangu wakati huo ameandika vitabu kadhaa vya utanzu huo. Kati ya hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Zawadi ya Slangens" (2014), "Dommer og bøddel" (2015), "Blodregn" (2016) na "Msafishaji" (2019).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    9.95 kr.

    Johan Boje, afisa wa jeshi la polisi la Eneo la Kati na Magharibi mwa Jutland, anauawa na dereva anayemgonga na kisha kutoroka mbele ya nyumba yake, usiku mmoja wa manane mwezi Machi. Bosi wake, Axel Borg, ni mmojawapo wa watu wa kwanza kuwasili katika eneo la tukio na hapa, anagundua kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kikatili. Mwanawe Johan Boje mwenye umri wa miaka tisa anasema kuwa aliliona gari na dereva, ambaye anadai alikuwa ni afisa wa polisi. Je, huu ni ubunifu unaofanana na ukweli wa mvulana huyo? Wakati kamera ya upelelezi inapothibitisha madai ya mwanawe, Roland Benito, mpelelezi katika Tume Huru ya Malalamishi ya Polisi, anapewa kesi hiyo. Je, mmoja wa marafiki za Johan alikuwa na nia ya kufanya mauaji hayo ya kinyama?Inger Gammelgaard Madsen (alizaliwa 1960) ni mwandishi Mdenmaki. Awali Madsen alikuwa msanifu picha. Alianza uandishi kwa riwaya iitwayo, "Dukkebarnet" mnamo 2008 na tangu wakati huo ameandika vitabu kadhaa vya utanzu huo. Kati ya hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Zawadi ya Slangens" (2014), "Dommer og bøddel" (2015), "Blodregn" (2016) na "Msafishaji" (2019).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    From 9.95 kr.

    Bertram anaogopa kuenda kwa polisi kuwaambia kuhusu kile alichokipata kwenye jaketi aliyoiba kwani yeye ni mhalifu anayesakwa na hataki jambo lolote linalihusiana na utekelezaji wa sheria. Jioni moja anajaribu kupiga simu bila kujitambulisha huku akiwa amelewa na baada ya kuvuta sigara kadhaa, ila polisi wanakataa kumuamini. Baadaye wakati Bertram anagundua kuwa maisha ya mama yake yamo hatarini, anajaribu kumuonya ila pia mama yake hamuamini. Bertram anaanza kumfuata mama yake na kutambua kuwa anakutana na mwanamume ambaye Bertram hamfahamu. Wakati Bertram anamuuliza mwanamume yule ni nani, mama yake hatimaye anakubali kuwa yule ni mpenzi wake na kuwa wanapanga kuondoka katika eneo lile na kuanza maisha mapya pamoja. Bertram anaamua kupekua ili kujua anapoishi mwanamume huyu, na kuvunja nyumba na kuingia ili kugundua yale atakayoweza kuhusu mwanamume huyu. Anapoangalia vitu vya mwanamume huyu, anapata mkusanyiko wa pasipoti ghushi, na picha ya mwanamume yule akiwa amevalia jaketi ile ambayo Bertram alikuwa ameiba.The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. Baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    From 9.95 kr.

    Habari mpya katika kesi hii inamfanya Roland kuangalia tena mauaji ya mlinzi yule wa jela. Kwa sasa ana uhakika kuwa anamfahamu Uwe Finch na anaamua kumfahamisha Anne Larsen. Anne ndiye alipata michoro ya vidole vya Uwe Finch, na kwa muda uliopita, Roland ametambua kuwa Anne anaweza kuwa mtu wa msaada mkubwa katika uchunguzi wa polisi. Bertram anashtuka kutambua kilichomfanyikia mama yake ila kwa mara moja Anne Larsen, mwanahabari kutoka TV2 East Jutland, anafika. Bertram anaangua kilio mbele ya Anne huku akimueleza mambo yote na Anne anamuambia kuwa wanahitaji kuondoka mara moja. Ila muda umeyoyoma. Wakati Roland anasikia kuhusu kifo kipya kupitia redio ya gari lake anahofia kuwa huenda Anne Larsen ako hatarini pia na anajaribu kumpigia simu ila hapati majibu. Anapopokea simu, anatumai kuwa ni Anne ila inageuka na kuwa ni Leif Skovby, ofisa mmoja katika kesi ile ya mauaji. Leif anataka kuonana naye Roland, na kile anachomwambia kinafanya mambo yote kubainika. Roland anamtumia ofisa huyu kumsaidia kupata simu ya Anne ila, je, Roland atampata Anne kabla ya muda kuyoyoma?The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. Baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    From 9.95 kr.

    Roland Benito, ambaye anakifanyia kazi Kitengo Huru cha Malalamiko kuhusu Polisi, ametumwa pamoja na mfanya kazi mwenza kwenda kuwahoji maafisa wawili wa polisi ambao wameitika mwito wa hali ya dharura. Mlinzi mmoja wa jela amejirusha kutoka kwa dirisha ya chumba chake kilicho katika orofa ya nne, punde tu maafisa hawa wawili wanapowasili baada ya kupata malalamishi kuhusu muziki wa sauti ya juu kutoka kwa chumba hicho. Kwa mtazamo wa juu, hakuonekani kuwa na jambo lolote la kukisiwa kuhusu hali hii ila pale inapotambulika kuwa mlinzi huyu wa jela ni baba ya rafiki wa dhati wa mjukuu wake Roland wanaosoma pamoja, Roland anasikia kuwa mfungwa mmoja amefariki kwenye jela pale alipokuwa akifanya kazi na kuwa mlinzi huyu wa jela amekuwa akihisi kutishiwa na anayefuatwa. Je, inawezekana kuwa haya hayakuwa mauaji ya binafsi hatimaye? Anne Larsen, mwandishi wa habari kutoka TV2 East Jutland, pia ananukuu hadithi ya vifo hivi. Wakati wa utafiti wake, anatambua kifo kingine, wakili wa utetezi aliyefariki katika ajali ya barabarani. Anatambua kuwa vifo hivi vyote vinahusishwa na mfungwa mmoja, Patrick Asp muuaji wa mtoto, ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumuua mtoto wake mdogo wa kike, na ambaye ni mfungwa katika jela ambayo mlinzi yule wa jela alikuwa akifanya kazi.The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

  • by Inger Gammelgaard Madsen
    From 9.95 kr.

    Bertram na marafiki wake watatu; Jack, Kasper na Felix, wamekamilisha masomo yao hivi punde na kutengeneza genge ndogo la muda na kujiita The Hawks. Wao wanamfanyia kazi The Handler, ambaye huwalipa baada ya wao kuvunja maduka na kuuba fanicha bainifu za bei ghali pindi The Handler anapopata agizo kutoka kwa wateja wake. Bertram anaishi yeye na mama yake pekee anayefanya kazi kama mhudumu katika mkahawa. Mamake Bertram anaamini kuwa Bertram anapata pesa zake kutokana na kuwasilisha magazeti. Bertram hawezi kukumbuka mambo mengi kuhusu baba yake. Alikuwa na miaka saba tu wakati baba yake alishikwa baada ya kutekeleza mauaji na kuhukumiwa kifungo cha maisha kwenye jela. Siku moja Bertram anaiba jaketi ya bei ghali iliyotengenezwa kwa ngozi kwenye mkahawa ambao mama yake anafanya kazi. Anapata kitu kilichofichwa katika mfuko ulijificha chini ya bitana ya jaketi ile. Hili linaishia kutokea kwa maafa na sio kwa Bertram tu.The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

  • by Jesper Nicolaj Christiansen
    9.95 kr.

    Mvulana anaamka katikati ya msitu. Hajitambui au kutambua jinsi alivyofika pale. Kwa usaidizi wa watu tofauti na wanyama, na pia mkuki ulio na uwezo wa kipekee, Ronin huyu anapitia matukio mengi. Wakati ambapo kijiji kinahitaji ulinzi wake, lazima ajifunze kupigana kwa heshima ya wakulima anaowaokoa, na kwa ajili yake mwenyewe.Mvulana anaamka msituni bila kukumbuka ya yeye ni nani au atokako. Kupitia mfululizo huu, Ronin anapitia matukio mengi ambayo yanamsukuma ukingoni. Njiani, anakutana na watu ambao wanamsaidia kukua na kujifunza mambo yaliyo muhimu. Kwa usaidizi wa mkuki wake wa ajabu na nguvu anazozipata kutoka kwenye mkuki huu, Ronin anapigana kwa wema. Kwa kila tukio jipya, Ronin anakaribia zaidi na zaidi kujitambua hakika yeye ni nani.Jesper Christiansen (b. 1972) ni mwandishi wa asili ya Kideni. Amehitimu katika Shule ya Uandishi wa Hadithi za Watoto na yeye huandika hadithi za matukio na za kubuni za watoto wa kila umri.

  • by Daniel Zimakoff
    9.95 kr.

    Mpira wa miguu sio kuhusu kuishi au kifo – ni muhimu sana!Jake, Nick, Peter, na wachezaji wengine FC Mezzi sasa wapo ligi kuu . kasi yao ni ya haraka, mashambulizi yao hayana mpangilio, na michezo inaonekana kuwa migumu zaidi kuliko hapo awali. Zaidi ya hayo, Nick na Zlatan wanagombana, na ikiwa hawatacheza kama timu, hawatakuwa na nafasi ya kushinda ligi. Je, Jake, ambaye ni nahodha, anaweza kufanya lolote kuhusu hilo? Na vipi kuhusu Ursula na Zlatan? Wanashirikiana?Mpira wa miguu sio kuhusu kuishi au kufa – ni muhimu sana! \n\nJake na marafiki zake walianzisha timu yao wenyewe, FC Mezzi. Tunafuatilia michezo yao ya mazoezi, mashindano na ya kirafiki ya zamani na mipya. Pia kuna mambo ya mapenzi kidogo. \n\nMfululizo huu unahusu kufurahia michezo!Daniel Zimakoff alizaliwa mwaka 1956 na mkutubi aliyesomea. Kwa mara ya kwanza mwaka 1980 aliandika mfurulizo mkubwa wa vitabu vya watoto na ashawahi kupata Tuzo ya Vitabu vya Watoto kuto kwenye wizara ya utamaduni.

  • by Jesper Nicolaj Christiansen
    9.95 kr.

    Katika sehemu ya mwisho ya mfululizo wa Ronin, Ronin anasafiri kwenda Meifumado kukutana na hatima yake na kuyaokoa maisha ya Azami. Ni kwa kupigana na Kivuli cha Mfalme na jeshi lake la mapepo wabaya ambapo Ronin anajifunza kuhusu mambo yake ya kale, familia yake na jinsi anavyoweza kutenda kulingana na jinsi alivyo na jinsi anavyoamini. Katika hali ngumu zaidi, lazima Ronin akumbuke jinsi shujaa wa kweli anavyopaswa kuwa.Mvulana anaamka msituni bila kukumbuka ya yeye ni nani au atokako. Kupitia mfululizo huu, Ronin anapitia matukio mengi ambayo yanamsukuma ukingoni. Njiani, anakutana na watu ambao wanamsaidia kukua na kujifunza mambo yaliyo muhimu. Kwa usaidizi wa mkuki wake wa ajabu na nguvu anazozipata kutoka kwenye mkuki huu, Ronin anapigana kwa wema. Kwa kila tukio jipya, Ronin anakaribia zaidi na zaidi kujitambua hakika yeye ni nani.Jesper Christiansen (b. 1972) ni mwandishi wa asili ya Kideni. Amehitimu katika Shule ya Uandishi wa Hadithi za Watoto na yeye huandika hadithi za matukio na za kubuni za watoto wa kila umri.

  • by Daniel Zimakoff
    9.95 kr.

    Mpira wa miguu sio kuhusu kuishi au kifo – ni muhimu sana!Jake, Nick, and Peter ni marafiki wakubwa. Wanapenda mpira wa miguu na wanacheza katika kilabu kimoja. Jake na Nick wanaingia ligi daraja la kwanza. Walikuwa na shauku kubwa! Walianzia nje kwenye michezo miwili ya kwanza, lakini Jake hakucheza sana kwenye mchezo wa kwanza. Na wakati zimesalia dakika kumi tu za mchezo wa pili, bado alitakiwa kucheza. Huu ni wakati ambao Jake anafanya maamuzi makubwa.Mpira wa miguu sio kuhusu kuishi au kufa – ni muhimu sana! \n\nJake na marafiki zake walianzisha timu yao wenyewe, FC Mezzi. Tunafuatilia michezo yao ya mazoezi, mashindano na ya kirafiki ya zamani na mipya. Pia kuna mambo ya mapenzi kidogo. \n\nMfululizo huu unahusu kufurahia michezo!Daniel Zimakoff alizaliwa mwaka 1956 na mkutubi aliyesomea. Kwa mara ya kwanza mwaka 1980 aliandika mfurulizo mkubwa wa vitabu vya watoto na ashawahi kupata Tuzo ya Vitabu vya Watoto kuto kwenye wizara ya utamaduni.

  • by Daniel Zimakoff
    9.95 kr.

    Mpira wa miguu sio kuhusu kuishi au kifo – ni muhimu sana!FC Mezzi inaenda Barcelona wakati wa likizo ya kiangazi. Wanaenda kuishi kwenye shule yenye bwawa, kucheza kwenye mashindano dhidi ya timu za Hispania, na kutembelea Camp Nou. Wana shauku kubwa. Hata wameweza kutimiza matamanio yao makubwa: Wakiwa wanaelekea Camp Nou wanakutana na Messi! Labda wanaweza hata kurudisha kombe nyumbani?Mpira wa miguu sio kuhusu kuishi au kufa – ni muhimu sana! \n\nJake na marafiki zake walianzisha timu yao wenyewe, FC Mezzi. Tunafuatilia michezo yao ya mazoezi, mashindano na ya kirafiki ya zamani na mipya. Pia kuna mambo ya mapenzi kidogo. \n\nMfululizo huu unahusu kufurahia michezo!Daniel Zimakoff alizaliwa mwaka 1956 na mkutubi aliyesomea. Kwa mara ya kwanza mwaka 1980 aliandika mfurulizo mkubwa wa vitabu vya watoto na ashawahi kupata Tuzo ya Vitabu vya Watoto kuto kwenye wizara ya utamaduni.

  • by Jesper Nicolaj Christiansen
    9.95 kr.

    Ronin anaendelea na safari yake ya kuelekea Meifumado. Njiani, anashambuliwa na maadui ambao ni waovu zaidi kuliko chochote ambacho aliwahi kukutana nacho. Akiungana na marafiki zaidi, analazimika kufanya uamuzi mgumu na kuvishinda vikwazo vyake vigumu zaidi.Mvulana anaamka msituni bila kukumbuka ya yeye ni nani au atokako. Kupitia mfululizo huu, Ronin anapitia matukio mengi ambayo yanamsukuma ukingoni. Njiani, anakutana na watu ambao wanamsaidia kukua na kujifunza mambo yaliyo muhimu. Kwa usaidizi wa mkuki wake wa ajabu na nguvu anazozipata kutoka kwenye mkuki huu, Ronin anapigana kwa wema. Kwa kila tukio jipya, Ronin anakaribia zaidi na zaidi kujitambua hakika yeye ni nani.Jesper Christiansen (b. 1972) ni mwandishi wa asili ya Kideni. Amehitimu katika Shule ya Uandishi wa Hadithi za Watoto na yeye huandika hadithi za matukio na za kubuni za watoto wa kila umri.

  • by Peter Gotthardt
    9.95 kr.

    Adui mwenye nguvu aliwasili kwenye nchi ya Vibwengo. Alitaka kumfanya mtumwa kila mtu anayeishi pale. Ikiwa Vibwengo wataokoka, watahitaji vyote ujasiri na matumaini.Mshauri wa Mfalme, Mchawi, amembaini Deizi na jeshi lote la Vibwengo. Mmea usionyauka na mama yake Deizi, Veronika, wanakuja kuwaweka huru. Lakini wataweza kuwapita wanajeshi wote wa Mfalme mwenye Majivuno na uchawi wa Mshauri wa Mfalme?Hiki ni kitabu cha nne katika mfululizo wa vitabu vinne vya "Hatima ya Vibwengo." Visome vitabu vyote katika mfululizo:Wanajeshi ShupavuMoyo wa JabaliMakaburi YaliyosahaulikaFilimbi ya KichawiPeter Gotthardt alizaliwa nchini Denmark karibu na Copenhagen mwaka 1946. Akiwa mtoto alipenda kusoma, na alitumia muda wake mwingi kujisomea katika maktaba za mkusanyiko wa vitabu vya historia na matukio. nnGotthardt ameandika zaidi ya vitabu 60 vya watoto ambapo vingi vimejikita kwenye uwanja wa Vibwengo.

  • by Peter Gotthardt
    37.99 kr.

    Adui mwenye nguvu aliwasili kwenye nchi ya Vibwengo. Alitaka kumfanya mtumwa kila mtu anayeishi pale. Ikiwa Vibwengo wataokoka, watahitaji vyote ujasiri na matumaini.Mkwamba unataka kusaidia wakati wa mapigano dhidi ya maadai wa Vibwengo. Lakini Deizi hakufikiria kuwa ni mkubwa vya kutosha. Mkwamba haujakata tamaa. Pamoja na Mzaha, Kijana wa Zimwi aliinyemelea kambi ya adui. Walikuwa na mpango. Lakini wataweza kuendelea kujificha dhidi ya Makonde ya Chuma na majitu ya kutisha ya mfalme?Hiki ni kitabu cha pili katika mfululizo wa vitabu vinne vya “Hatima ya Vibwengo.” Visome vitabu vyote katika mfululizo:Wanajeshi ShupavuMoyo wa JabaliMakaburi YaliyosahaulikaFilimbi ya KichawiPeter Gotthardt alizaliwa nchini Denmark karibu na Copenhagen mwaka 1946. Akiwa mtoto alipenda kusoma, na alitumia muda wake mwingi kujisomea katika maktaba za mkusanyiko wa vitabu vya historia na matukio.Gotthardt ameandika zaidi ya vitabu 60 vya watoto ambapo vingi vimejikita kwenye uwanja wa Vibwengo.

  • by Daniel Zimakoff
    9.95 kr.

    Mpira wa miguu sio kuhusu kuishi au kifo – ni muhimu sana!FC Mezzi wanaanza muhula mpya, na lazima wajifunze kucheza tisa kila upande. Ni aina mpya ya mchezo kwenye wanja mkubwa na kanuni za kuotea. Wanamiliki hata nyumba ya kilabu, na wanaizindua kwa They even have their own clubhouse, and they are consecrating it with a horror sleepover. Jake akaushika mkono wa Ursula gizani. Je, anakuwa mpenzi wake wa kwanza? Kisha anasikia kwamba wasichana wanafikiria kuondoka kwenye timu ili kiucheza tenisi. Ghafla Jake anaacha kutenda kama nahodha halisi.Mpira wa miguu sio kuhusu kuishi au kufa – ni muhimu sana! \n\nJake na marafiki zake walianzisha timu yao wenyewe, FC Mezzi. Tunafuatilia michezo yao ya mazoezi, mashindano na ya kirafiki ya zamani na mipya. Pia kuna mambo ya mapenzi kidogo. \n\nMfululizo huu unahusu kufurahia michezo!Daniel Zimakoff alizaliwa mwaka 1956 na mkutubi aliyesomea. Kwa mara ya kwanza mwaka 1980 aliandika mfurulizo mkubwa wa vitabu vya watoto na ashawahi kupata Tuzo ya Vitabu vya Watoto kuto kwenye wizara ya utamaduni.

  • by Peter Gotthardt
    9.95 kr.

    Adui mwenye nguvu aliwasili kwenye nchi ya Vibwengo. Alitaka kumfanya mtumwa kila mtu anayeishi pale. Ikiwa Vibwengo wataokoka, watahitaji vyote ujasiri na matumaini.Mahali fulani ndani sana kwenye mlima kuna fimbo takatifu ambayo inaweza kumzidi nguvu Mfalme mwenye Majivuno, ambaye ni adui mbaya zaidi wa Vibwengo. Lakini hakuna anayejua ilikofichwa. Je, Mkwamba na Rafiki zake wanaweza kuipata sehemu ilikofichwa kabla hawajachelewa?Hiki ni kitabu cha tatu katika mfululizo wa vitabu vinne vya "Hatima ya Vibwengo." Visome vitabu vyote katika mfululizo:Wanajeshi ShupavuMoyo wa JabaliMakaburi YaliyosahaulikaFilimbi ya KichawiPeter Gotthardt alizaliwa nchini Denmark karibu na Copenhagen mwaka 1946. Akiwa mtoto alipenda kusoma, na alitumia muda wake mwingi kujisomea katika maktaba za mkusanyiko wa vitabu vya historia na matukio. nnGotthardt ameandika zaidi ya vitabu 60 vya watoto ambapo vingi vimejikita kwenye uwanja wa Vibwengo.

  • by Peter Gotthardt
    37.99 kr.

    Adui mwenye nguvu aliwasili kwenye nchi ya Vibwengo. Alitaka kumfanya mtumwa kila mtu anayeishi pale. Ikiwa Vibwengo wataokoka, watahitaji vyote ujasiri na matumaini.Vibwengo walilikimbia jeshi la adui, na walilazimishwa kujificha msituni. Deizi akawa rafiki wa Kibwengo mdogo anayeitwa Humulus. Kwa pamoja, wakafanya ugunduzi ambao uliwawezesha Vibwengo kujibu mashambulizi dhidi ya adui. Je, watakuwa na nguvu ya kutosha?Hiki ni kitabu cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vinne vya “Hatima ya Vibwengo.” Visome vitabu vyote katika mfululizo:Wanajeshi ShupavuMoyo wa JabaliMakaburi YaliyosahaulikaFilimbi ya KichawiPeter Gotthardt alizaliwa nchini Denmark karibu na Copenhagen mwaka 1946. Akiwa mtoto alipenda kusoma, na alitumia muda wake mwingi kujisomea katika maktaba za mkusanyiko wa vitabu vya historia na matukio.Gotthardt ameandika zaidi ya vitabu 60 vya watoto ambapo vingi vimejikita kwenye uwanja wa Vibwengo.